Umoja wa Mataifa
@UmojaWaMataifa
Akaunti rasmi ya Umoja wa Mataifa. Kwa amani, utu & usawa katika ulimwengu wenye ustawi.
ID:67706757
https://news.un.org/sw/ 21-08-2009 20:15:32
34,4K Tweets
28,6K Followers
650 Following
Takriban waandishi wa habari 1,000 wameuawa katika muongo mmoja uliopita.
Visa 9 kati ya 10 kati ya hizo bado hazijasuluhishwa.
UNESCO inaeleza nini kinapaswa kufanyika ili ku #ProtectJournalists .
unesco.org/en/safety-jour….
'Watendee wengine kama unavyotaka kutendewa.'
-- Mchoro wa 'Golden Rule' katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umechorwa na msanii wa Marekani Norman Rockwell.
Siku ya Jumatatu #SikuYaSanaaDunia , tunasherehekea uwezo wa sanaa wa kutufariji wakati wa dhiki na kututia moyo.
Michezo ni chombo chenye nguvu cha kuimarisha uhusiano wa kijamii na kurejesha mazungumzo wakati wa mivutano ya kisiasa, kitamaduni au kidini.
Leo Jumamosi, ungana nasi kusherehekea #SportsDay na nguvu ya michezo kwa amani na maendeleo. un.org/en/observances…
Kila siku, watu hufa au kupoteza viungo kwa kukanyaga mabomu ya ardhini, na wengi wao ni raia katika maeneo yaliyopata amani.
Jumanne #MineAwarenessDay ni fursa ya kuangazia haja ya dharura ya kutokomeza mabomu ya ardhini. un.org/en/observances… v UNMAS #MineActionCannotWait
Elimu ni muhimu ili kuhakikisha kwamba vijana wananufaika kwa kupata maarifa zaidi kuhusu mazingira. Pitia zana za #GenerationRestoration ili kupata maarifa na nyenzo za kuboresha mifumo ya ekolojia. bit.ly/3FIv3LD
📸Ubunifu wa aina yake jijini Dar es Salaam, #Tanzania .
Tusipobadili tabia zetu, taka za plastiki zitakuwa nyingi baharini kuliko samaki🐟🐠.
Leo siku ya #ZeroWaste , fahamu jinsi unavyoweza #BeatPlasticPollution .
unep.org/events/un-day/…
Je wajua, chakula kinachoharibiwa nyumbani ni takribani milo bilioni 1 kwa siku?
Ripoti ya #FoodWasteIndex iliyotolewa na UNEP inaonyesha kiwango cha chakula kinachoharibiwa kote duniani na tunachoweza kufanya ili ku- #KomeshaTakaYaChakula : unep.org/sw/resources/m…
Unyogovu unaweza kutokea kwa mtu yeyote. Ni ugonjwa, si udhaifu wa tabia -- na unaweza kutibiwa.
World Health Organization (WHO) ina mwongozo kuhusu hatua za kuchukua ikiwa wewe au mtu unayemjali anaugua huzuni. bit.ly/2BGouav
Jinsi ya #Kupambana na Ubaguzi.
📖 Jielimishe kuhusu njia nyingi za ubaguzi wa rangi huumiza jamii
💭 TAFAKARI kuhusu suluhu za kutokomeza ubaguzi wa rangi.
🌱 PANDA maadili ya uvumilivu katika jamii yako yote.
Mawazo zaidi Jumatatu #RememberSlaveryDay : un.org/en/fight-racism
Utokeaji wa El Niño mwaka wa 2023-24 unapoanza kupungua, athari zake duniani zinaendelea kudumu. Gundua jinsi hali hii inavyoendelea kuongeza viwango vya joto na hali mbaya ya hewa, licha ya kupungua kwake polepole. Pata taarifa za sasa kutoka kwa
World Meteorological Organization: wmo.int/media/news/el-…
Je wajua, kuna ongezeko la uhaba wa maji duniani?
Masuluhisho yanahitaji utashi wa kisiasa, kuimarisha ukusanyaji wa data na ubia wa kukuza mikakati jumuishi ya kusimamia maji.
#SikuYaMajiDuniani , pitia masuluhisho ya kudumisha kuwepo kwa maji safi: bit.ly/3TO1b82
Misitu ni muhimu kwa afya ya sayari na ustawi wa binadamu.
Pia ni muhimu kwa kuendeleza uzalishaji wa chakula.
Siku ya Alhamisi ya Misitu Duniani, jifunze zaidi kutoka kwa Food and Agriculture Organization kuhusu umuhimu wa misitu endelevu. bit.ly/2TdyzlN
Kuhifadhi misitu ni mojawapo ya njia mwafaka za kukabiliana na #ClimateCrisis . Tunapoelekea #SikuYaMisitu , fahamu jinsi UNEP inavyofanya kazi kuhifadhi na kuboresha mifumo ya ekolojia ya misitu #KwaManufaaYaWatuNaSayari : decadeonrestoration.org/types-ecosyste…
Wanawake na wasichana wanasaidia kujenga ulimwengu bora kupitia uongozi wao katika...
🌱kuhifadhi mazingira
🌱kilimo
🌱nishati mbadala
🌱 #ClimateAction
Kama mawakala wa mabadiliko, lazima kwa usawa wawe sehemu ya suluhisho kuelekea mustakabali endelevu: bit.ly/3PPVQrg