NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

51 Hawajapatikana Mai Mahiu:

Idadi ya watu waliofariki katika mkasa wa mafuriko ya Mai Mahiu imefika 52 huku watu walipotea ikiwa 51.

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Waathiriwa Wa Mai Mahiu

Wakenya wajitokeza kuwapikia waathiriwa wa mkasa wa maji, kuwapa ushauri nasaha na hata kutenga maeneo ya watoto kucheza.

Nuru AbdulAziz George Kieru

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Afueni Ya Leba Dei

Rais Ruto atangaza nyongeza ya mshahara wa chini kwa 6%, japo kwa masharti.

Hili limewakera wafanyakazi waliohudhuria sherehe hizi za leba za 59.

Nuru AbdulAziz Lofty Matambo

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Wawili Wafariki Kitengela

Watu wawili wamefariki Kitengela kutokana na mafuriko.

Baadhi ya barabara pia zimesalia mahame baada ya kufurika na mito kuvunja kingo zake.

Nuru AbdulAziz

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Kampuni Ya Mnada Wa Magari:

Rais Ruto amezindua kampuni ya mnada wa magari kutoka Japan huko Naivasha.

Kampuni hii ni ya kwanza hapa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.

Nuru AbdulAziz

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Shambulizi La Kigaidi Elwak

Watu watano wameuawa leo huko Elwak Kaunti ya Mandera kufuatia mlipuko wa bomu aina ya IED.

Nuru AbdulAziz

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Kipi Kilochangia Gharika Mai Mahiu:

NTV yafika hadi chanzo cha maji yaliyosababisha maafa ya watu zaidi ya 45 Nakuru.

Wanajiolojia wasema janga la Maai Mahiu limetokana na kuungana kwa maporomoko ya ardhi awali.

Nicholas Wambua

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Ukiingia Raha, Ukitoka Wezi!

Kuna kundi jipya la vijana limechipuka Mombasa ambalo sasa linawalenga wakazi wanaotoka kununua bidhaa zao katika maduka makuu, ili kuwapora bidhaa zao.

Kevin Mutai

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Simulizi Za Manusura Mai Mahiu

Zaidi ya watu 70 wamefariki baada ya kusombwa na maji eneo la Maai Mahiu, Nakuru.
Zaidi ya majeruhi 100 wanatibiwa katika hospitali kadha wa kadha katika kaunti hiyo.

Brygettes Ngana

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Je, Wajua?

Mbwa wana alama za kipekee za pua zinazotumika kwa utambulisho.

Mbwa wanaweza kugundua magonjwa fulani na kupata watu waliopotea.

Je, Wajua?

Mbwa wana alama za kipekee za pua zinazotumika kwa utambulisho.

Mbwa wanaweza kugundua magonjwa fulani na kupata watu waliopotea.

#NTVJioni
account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Mvua Ya Mauti

Isaac Mwaura: Zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha yao kutokana na mafuriko yanayoshuhudiwa nchini.
Miili sita imepatikana katika eneo la Mathioya, Muranga baada ya mporomoko wa ardhi.

Hellen Aura🇰🇪

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Tahadhari Ya Mvua Kubwa:

Rais Ruto ameongoza kikao cha dharura kukabiliana na mafuriko yanayoendelea kote nchini.

Watu zaidi ya 1,000 wameachwa bila makao na wengine zaidi ya 10 kufariki.

Fridah Mwaka Fatuma Bugu

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

KDF Kuongoza Operesheni Mai Mahiu:

Serikali imesema kuwa itawajengea upya nyumba watu walioathiriwa na janga hilo ambapo watu 48 wamefariki kufikia sasa.

Nicholas Wambua

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Utoaji Wa Vitambulisho

Serikali imetangaza kwamba kuna mpango wa kutupilia mbali kamati za kutathmini utoaji wa vitambulisho nchini.

Nuru AbdulAziz

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Fidia Ya Mbolea Feki:

Serikali imeamuru kwamba wakulima waliouziwa mbolea ghushi na NCPB wapewa mbolea mbadala.

Hata hivyo, mbona serikali ikaamua kujitwika jukumu hilo ilhali kampuni iliyopewa kandarasi ya kuagiza mbolea ilikuwa ni ya kibinafsi.

Fridah Mwaka

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Siku Za ‘Nuhu’, Bingu Zafunguka

Watu watatu wameaga dunia kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha Meru.
Hali tete inaendelea kukumba maeneo tofauti nchini kufuatia mvua ya masika ambayo imesababisha mafuriko.

Fatuma Bugu

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Mafuriko Yasababisha Maafa:

Zaidi ya watu 12 wameaga dunia katika kaunti ya Nairobi na Kajiado kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Wakazi wa mitaa mbalimbali nchini wanakadiria hasara.

Nuru AbdulAziz Fatuma Bugu

account_circle